Thursday , 4th Aug , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amelitaka Shirika la umeme TANESCO, kufika shule za bweni, na kukagua mfumo uliotumika kuweka umeme na kuurekebisha ili kuondokana na tatizo la hitilafu ya umeme linalopelekea majanga ya moto.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda.

Ntibenda ameyasema hayo jana wakati akitembelea shule hiyo amesema kuwa japokuwa chanzo cha moto bado hakijajulikana ila hitilafu ya umeme imetajwa kuchangia tatizo hilo ambalo limepelekea baadhi ya wanafunzi kurudishwa majumbani baada ya vifaa vya kuharibiwa na moto.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wamerudishwa majumbani kwa siku saba ili kutafuta mahitaji yao na sehemu mbadala ya malazi watakayoitumia baada ya kurejea hivyo ameiomba jamii na mashirika mbalimbali kujitokeza kuisaidia shule hiyo.

Wanafunzi wa kidato cha Nne katika shule hiyo Muyo Jacob na Lomnayaki Mitawas wameiomba serikali na na jamii iwasaidie ili wenzao walioko majumbani waweze kurejea kwani wanakabiliwa na mtihani wa kidato cha nne ulioko mbele yao..

Matukio ya kuungua kwa bweni la shule ya Sekondari Lowassa, yamekua yakitokea mfululizo kwani kwa kipindi cha mwezi wa kwanza mwaka huu Bweni moja liliteketea kwa moto na baada ya miezi saba tukio lingine limetokea,suluhu ya kudumu inahitajika kuzuia matukio haya.