Thursday , 1st May , 2014

Rapa mkali kutoka nchini Kenya, STL ameendelea kupiga hatua za mafanikio ya muziki wake na kuuvusha mipaka, ambapo safari hii mwanadada huyu amepata mkataba wa kimataifa wa kusambaza na kusimamia kazi zake za muziki kutoka Universal Records.

STL

Mkataba huu wa STL ambaye kwa sasa anafanya poa katika chati mbalimbali na ngoma yake inayokwenda kwa jina Coolio, tayari umeshatiwa saini na pande zote mbili huko nchini Norway ambapo ndipo makazi mengine ya mwanadada huyu.

Mkataba huu unazifanya kazi za STL kuwa katika ngazi moja ya usimamizi na zile za wasanii wa kimataifa kama J Cole, Rihanna na Shakira ambao pia wanasimamiwa kazi zao na Universal Records.

Tags: