Tuesday , 26th Jul , 2016

Baada ya serikali ya Sudan Kusini kufungua mipaka yake kwa wanaotoroka mapigano nchini humo, takribani wakimbizi elfu 30 wamepokelewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, na wadau wake nchini Uganda.

Wakimbizi kutoka Sudan Kusini

UNHCR, inasema watu 24,321 waliingia Uganda kupitia mipaka ya Oraba, Elegu, Lamwo na Moyo, katika siku sita zilizofuata kufunguliwa kwa mipaka, na kwamba asilimia tisini yao ni wanawake na watoto.

Ilipofikia Ijumma wiki jana, jumla ya wakimbizi 26,468 walikuwa wametorokewa Uganda tangu kuibuka kwa mzozo wa kijeshi, tarehe saba mwezi huu jijini Juba.

Baadhi ya wanaosaka hifadhi wanadai kukimbia visa vya uporaji na wavulana kulazimishwa kujiunga na vikundi vya wapiganaji hasa katika maeneo ya Magwi, Jimbo la Eastern Equatoria.