Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akikagua Majeshi ya Usalama nchini humo
Ripoti iliyotolewa jana na shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch inasema kuna angalau visa 34 vya watu kuvamiwa na vyombo vya usalama na baadaye kutojulikana walipo au maiti zao kupatikana mbali na maeneo waliyokamatiwa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya, Mwenda Njoka, amekanusha tuhuma hizo, akisema lazima kwanza ripoti hiyo ichunguzwe na mamlaka ya kusimamia polisi nchini humo.
Mkurugenzi mtendaji wa Human Rights Watch, Ken Roth, amesema kuwaandama washukiwa, kuwakamata na kisha kukataa kutoa taarifa zinazowahusu, kunazidi kuwanyima wananchi imani kwa vyombo vya usalama vya Kenya.
Matukio ya aina hiyo yameripotiwa katika mji mkuu, Nairobi, na eneo la kaskazini mashariki, linalopakana na Somalia