Mbu ni mmoja wa wadudu wanaosambaza ugonjwa hatari wa homa ya Dengu
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Masuala ya Tiba katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dk. Kaliemeli John Wandi wakati alipokuwa akizungumza na EATV juu ya hali ya ugonjwa wa homa ya dengue kwa wagonjwa wanaofikishwa hospitalini hapo.
Amesema wengi wa wagonjwa hao wanatokea katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni na kueleza kwamba hali ya wagonjwa wa dengue huwa ni mbaya kutokana na wagonjwa hao kutokwa na damu nyingi katika sehemu za puani, masikioni na hivyo kusababisha kufariki dunia.