Sunday , 10th Jul , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amesema Tanzania itashirikiana na nchi ya India katika shuguli mbalimbali za kimaendeleo na kukuza viwanda.

Akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kusaini mikataba ya kimaendeleo baina ya Tanzania na India, Mhe. Magufuli amesema Tanzania inamengi yakuiga kwa nchi hiyo kwani ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa kwa kuwa na viwanda.

Miradi hiyo ambayo serikali imeiingia makubaliano na India, ni pamoja na mradi wa kusambaza maji upande wa Pwani na Dar es Salaam, Mkopo kwa serikali kw aajili ya kusambaza maji upande wa Zanzibar na utoaji wa mashine ya vipimo vya ugonjwa wa saratani.

Rais Magufuli ameongeza kuwa, India itashirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu, kufanya utafiti na kuendeleza miradi na sekta ya viwanda vidogo vidogo, kuanzisha vituo vya utamizi kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kiteknolojia kwa wabunifu wa kitanzania jambo ambalo litaiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda.

“Asilimia 80 ya bajetiyzetu tunatumia kununua madawa, India itatusaidia kuondokana na hilo kwakuleta vifaa na wataalamu wa kuzalisha dawa hapa nchini kwetu watusaidie. Pia India ni wazuri kwa masuala ya Tehama kwa hilo watatuwezesha kurekebisha mifumo yote ya serikali kuwa katika mfumo mmoja,” amesema rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa India Bw. Narendra Mondi amesema mbali na mikataba mipya iliyo sainiwa, India imewekeza nchini miradi ya dola bilioni tatu za kimarekani kwa nia moja ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo.