Akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama sabasaba, Mfanyabiashara kutoka TWC bi. Consolata Lwegasira amesema watanzania wamekuwa na mwamko mdogo wa kununua bidhaa zitokanazo na madini ya Tanzania kwakutojua aina za madini hayo na bidhaa zitokanazo na madini hayo.
Aidha, Bi. Consolata amesema endapo serikali itawekeza katika kutangaza madini ya Tanzania kwa wananchi wake na kimataifa nidhahiri kuwa itachangia kuongea pato la taifa kwa kasi na kukuza uchumi.
Hata hivyo Consolata ameiomba serikali kupitia wizara husika kuhakikisha inawezesha wanawake waliopo katika sekta ya uchimbaji madini hasa wale wachimbaji wa kati ili waweze kujiendeleza kwa ufasaha katika shughuli zao za uchimbaji na kuondokana na changamoto nyingi zinazowakabili.


