Monday , 28th Apr , 2014

Baada ya tetesi za kutokea mpasuko ndani ya kundi la P Square kuchukua nafasi kwa siku kadhaa sasa, taarifa mpya inayoashiria kuwa kwa sasa mambo yapo shwari kati ya Peter na Paul imeibuka hasa baada ya wawili hawa kuonekana hadharani kwa pamoja.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Peter na Paul kuonekana hadharani baada ya ugomvi kati yao kuripotiwa na kuzua wasi wasi mkubwa kwa mashabiki wa kundi hili juu ya kutengana kwao wakati wakiwa katika kilele cha mafanikio.

Chanzo cha taarifa za kuwepo kwa ugomvi katika kundi hili kilikuwa ni ujumbe wa meneja na kaka wa damu wa wasanii hawa, Jude Okoye kutangaza mtandaoni kuwa baada ya miaka mingi ya mafanikio anaona kuwa sasa imetosha.

Tags: