Tuesday , 28th Jun , 2016

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, imezindua awamu ya pili ya mpango wa usaidizi maendeleo UNDAF uanolenga kusaidia kusukuma mbele juhudi za maendeleo katika sekta tofauti nchini humo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome.

Wakiongea baada ya uzinduzi huo mjini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome ameelezea namna taifa litakavyonufaika na mpango huo.

Mchome amesema kuwa moja kati ya masuala ambayo nchi itafaidika nayo ni pamoja na sekta ya za kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Zanzibar Khamis Musa anazungumzia namna mpango wa awali ulivyofanikiwa ikiwemo huduma za afya kwa mama na mtoto zimeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Zaidi ya dola bilioni moja za Marekani zimetengwa kwa ajili ya mpango huo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa awamu ya pili UNDAF.

Sauti ya Katibu Mkuu wa wizara ya elimu Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome.