Wednesday , 15th Jun , 2016

Baada ya kimya kirefu kutokana na kuanza majukumu ya kuwa mama wa familia, msanii Pipi leo amefunguka na kuelezea ni jinsi gani anakabiliana na jukumu hilo, na kazi yake ya muziki.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Pipi amesema hapati ugumu mkubwa kwenye malezi ya watoto hao na kazi yake ya muziki, kwani mume wake na familia yake wanampa msaada mkubwa.

"Haina uzito wowote kwa sababu mume wangu ndiye ambaye ananisapoti, lakini pia mi bahati nzuri bado yupo hai, wakwe zangu wote bado wapo hai kwa hiyo muda mwengine ambao watoto wanakuwa kama baba yao anakuwepo, yupo comfortable kubaki nyumbani na watoto, au na wazazi wangu au na wake zangu, kwa hiyo sipati sana shida kwamba watoto wananisumbua, hapana, some times naenda na watoto wangu kazini kwangu", alisema Pipi.

Pipi ambaye hivi sasa ameachia kazi mpya, amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kwani anarudi rasmi kwenye game, baada ya kimya hicho kirefu.