Tuesday , 14th Jun , 2016

Uwezo binafsi na ubunifu wa kiwango cha hali ya juu alionao kiungo mkabaji wa Leicester City na Ufaransa Kante umemkuna kocha wa Manchester United Jose Mourinho na sasa amemweka katika mahesabu yake ya usajili wa msimu ujao ili kuimarisha timu hiyo.

Kiungo wa Leicister City N’Golo Kante.

Pamoja na uwepo wa viungo kama Michael Carrick, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin na Daley Blind, kocha Mourinho bado ameona hakuna mkabaji wa staili anayotaka kwa sasa.

Mourinho ambaye kwa sasa akishirikiana vema na kwa ukaribu na maskauti wa timu ya Manchester United ameendelea kutazama michuano mikubwa ambayo inaendelea hivi sasa ya Copa Amerika na ile ya Euro ambayo inahusisha nyota wengi wakiwango cha dunia.

Kante ameendelea kuonyesha cheche na uwezo wake wa hali ya juu wa kukaba akiiwezesha Ufaransa ambao ni wenyeji wa michuano ya Euro kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo dhidi ya Romania na timu yake kushinda kwa bao 2-1.

Katika kuangalia michuano hiyo kocha huyo ambaye anasifika kwa kucheza soka la kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza amemwona kiungo mkabaji wa timu ya Leicister City N’Golo Kante raia wa Ufaransa na kuanza kuumizwa kichwa na uwezo wa kiungo huyo aliyekatika kiwango bora kwa sasa barani Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuharibu na kujenga mashambulizi.

Mourunho amekiri kukubali uwezo wa kiungo huyo mwenye miaka 25 akimfananisha na kiungo wa zamani wa Chelsea raia wa Ufaransa Claudio Makhelele ambaye Enzi za uchezaji wake alikuwa fundi wa kukaba na kuharibu mipango ya viungo na wahsambuliaji wa timu pinzani na hivyo kushabihiana kwa kila kitu na kiungo huyo fundi aloiyeiwezesha Leicister City kutwaa ubingwa wa kwanza wa kihistoria wa ligi kuu ya England EPL msimu huu.

Uamuzi wa Mourinho unaweza kuwa ni tiba katika eneo la kiungo mkabaji la United kufuatia eneo hilo kuwa kama ugonjwa usiona dawa tangu kuondoka kwa Mscotish Sir Alex Ferguson na pamoja na Mtangulizi wake Luis Van Gaal kuwatumia kina Michael Carrick na wengineo lakini eneo hilo bado lilikuwa changamoto kubwa kwa mafanikio duni ya United kwa misimu kadhaa sasa na hivyo ni wazi Mreno huyo atakuwa akipigana kwa kila njia ili kuhakikisha Kante anatua katika viunga vya Old Trafold msimu ujao.

Uwezekano wa Mourinho kusaka saini ya kiungo huyo mfupi mwenye mapafu ya mbwa nunatokana na hali ya usajili wa viungo kama Tony Kloos na Paul Pogba kuonekana kuwa ngumu kwa United hasa kutokana na dili hilo kuingiliwa na vigogo wengine wa Ulaya Real Madrid ya Hispania ambao wanamhitaji Pogba huku Kloos yeye akihitajika na Juventus ya Italia.