
Naibu Waziri ameyasema hayo Bungeni wakati wa maswali na majibu, wakati alipoulizwa swali na Mbunge wa Viti Maalumu Vicky Kamata kuhusu wananchi wanaozunguka mgodi huo faida wanazopata ikiwa ni pamoja na kufahamu faida ya wananchi ambao walitoa maeneo yao kwa ajili ya mgodi huo kuweza kuchimba madini.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Dkt. Kalemani amewema kwamba mgodi wa geita ulipewa leseni na serikali ya kuchimba eneo la kilomita 196 ambapo mgodi huo pia ulifanya mazungumzo na wananchi waliokuwa wanazunguka eneo hilo na kuwalipa fidia na kuchimba maeneo yao.
Kuhusu faida ambazo mgodi huo umetoa kwa wananchi Naibu Waziri amesema mgodi huo umesaidia kujenga miradi ya maji, afya na elimu katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutoa ajira kwa watanzania 1568 katika kazi mbalimbali.