Monday , 6th Jun , 2016

Bingwa wa mchezo wa Kickboxing hapa nchini Japhet Kaseba amewataka Mabondia kuachana na njia rahisi ili kuweza kushinda katika mapambano mbalimbali.

Kaseba amesema, mabondia wanatakiwa kukubali kupambana ili kuweza kushinda kwa nguvu zao na sio kununua mechi au kutengenezewa matokeo ili kuweza kushinda.

Kaseba amesema, kutengenezewa matokeo au kununua mechi inapelekea bondia anakuwa muoga na anashindwa kujiamini kwasababu anajua kabisa pambano analotakiwa kupambana na kubwa na hawezi kulinunua.

Kaseba amesema, bondia anapojiamini anauwezo wa kupambana an bondia yoyote Yule bila kujali anatoka nchi gani au amepambana na kushinda mapambano mangapi.