Thursday , 2nd Jun , 2016

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo wanaonufaika na mikopo ya mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa ya Kinondoni .

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo wanaonufaika na mikopo ya mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa ya Kinondoni .

Akiongea na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Sebastian Mhowera amesema kuwa maonesho hayo yanalenga kuwapa fursa wajasiriamali wadogowadogo kuonyesha shughuli wanazoziofanya na kutangaza Bidhaa zao .

Aidha jumla ya vikundi 546 vyenye jumla ya wajasiriamali 2729 wanaojishughulisha na kilimo, biashara ndogondogo, ushonaji,ufugaji, uvuvi, fundi selemala, ususi,usafi na bodaboda wataonesha shughuli zao katika viwanja vya Biafra ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Meya wa manispaa ya Kinondoni.