Tuesday , 31st May , 2016

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonyesha kusikitishwa na hatua ya serikali ya kuwafukuza katika majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wanafunzi wa chuo hicho ndani ya saa 24 kwa kutumia vyombo vya dola.

Akitoa tamko la kituo hicho Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Helen Kijo-Bisimba, amesema kitendo cha serikali kuwapeleka polisi wenye mabomu ya machozi na silaha ili kuwatawanya wanafunzi hao ni cha ukiukaji wa haki za binadamu kuwahi kufanywa ndani ya nchi inayozingatia Demokrasia.

Amesema kuwa wanafunzi hao wameadhibiwa kwa makosa yasiyo yao kwani kama ni tatizo lilikuwa ni kati ya serikali na wahadhiri ambao waliogoma wakidai stahiki zao, na kuhoji kwanini waadhibiwe wanafunzi wasio na hatia na serikali hii ambayo imeapa kuwatetea wananchi wake.

Dkt. Kijo-Bisimba amesema ameshangazwa na serikali kwani hata baadhi ya wabunge walipojitokeza bungeni kuwatetea wanafunzi hao ambao wanataabika mitaani Dodoma baada ya kutimuliwa chuo, walionekana maadui na kuchukuliwa uamuzi wa kikao cha bunge kuharishwa ili kuzizima sauti zao.