Monday , 30th May , 2016

Mshambuliaji kinda wa Manchester United, Marcus Rashford amesaini mkataba mpya wa miaka 4 na klabu hiyo ya Old Trafford.

Mshambuliaji kinda wa Manchester United, Marcus Rashford, amesaini mkataba mpya wa miaka 4 na klabu hiyo ya Old Trafford.

Uwezo wa kupachika mabao wa kijana huyo ndiyo umewavutia viongozi wa United kumwongezea mkataba, baada ya kufunga mabao 8 katika mechi 18 alizochezea kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari mwaka huu.

"Nina furaha sana kusaini mkataba mpya. Siku zote nimekuwa shabiki wa Manchester United, hivyo kucheza kwenye kikosi cha kwanza, kiukweli ni ndoto iliyokuja kutimia," Rashford aliiambia tovuti ya klabu.