Monday , 30th May , 2016

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia vijana 33 wa kundi maarufu kwa jina la Panya Road kwa kosa la kufanya matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro, amesema kuwa vijana hao wanatabia ya kuibuka na kupoketea hali iliyokuwa ikilisumbua sana jeshi la polisi ma ndipo polisi wakaandaa oparasheni maalum iliyofanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 15 kutoka Temeke na 18 kutoka Ilala.

Kamanda Sirro amesema kuwa vijana waliokamatwa ni wenye umri kati ya miaka 15 na 17 hivyo ni watoto ambao walitakiwa kuwa chini ya uangalizi wa mzazi sasa ni jukumu la wazazi kuahakikisha kuwa wanakuwa na uangalizi mzuri kutoka kwa watoto wao.

Aidha, Kamanda Sirro amesema kuwa wahalifu wote watakaokamatwa kutokana na makosa mbalimbali watafuatiliwa mali wanazomiliki na endapo itabainika kuwa zimepatikana kwa njia ya wizi watataifishiwa mali hizo.