Shamba la Ngano
Mtafiti Mwandamizi wa mbegu nchini na Mratibu wa Mradi wa uimarishaji Utafiti wa uendelezaji wa Ngano barani Afrika (SARD), Dkt. Rose Mongi amesema wakulima nchini Tanzania tani wanazozalisha ni sawa na asilimia 10 ya ngano yote inayohitajika nchini.
Mongi amesema kutokana na wakulima kuzalisha kiasi kidogo cha Ngano,serikali inalazimika kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza asilimia 90 ya ngano kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji halisi ya bidhaa kwa mwaka.
Bi. Mongi amesema hayo wakati alipotembelea na kukagua mashamba ya wakulima wa ngano katika vijiji vya wilaya ya Nkasi na Sumbawanga mkani Rukwa wanaolima chini ya uangalizi na ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu na watafiti wa mradi wa ngano.