Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Akizungumza jana visiwani humo na viongozi wa halmshauri ya CCM za mikoa miwili ya kisiwani wa Pemba, Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd, aliwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatia za kisheria watumishi wanaofanya vitendo vya ubaguzi.
Balozi Seif amesema kuwa serikali aitavumilia vitendo vya vya ubaguzi wa aina yoyote ikiwa wananchi kubaguliwa katika kupata huduma muhimu za kijamii na kuwataka kuchukua hatua za kuwafichua watu wanaofanya vitendo hivyo.
Aidha, Mhe. Balozi Seif, amesema kuwa licha ya uchaguzi kupita serikali kupitia vyombo vya dola italazimika kuimrisha zaidi ulinzi ili kuwapa fursa pana wananchi waendelee kupata fursa na uwezo wa kuishi kwa amani na utulivu.