Tuesday , 17th May , 2016

Ngumi ni mchezo unao kuwa kwa kasi nchini lakini mabondia wamekuwa wakikosa vifaa vya mazoezi, ulingo na ukumbi za kisasa kwa ajili ya mapambano ya ndani na kimataifa.

Kushoto ni ukumbi wa MGM Grand maarufu kwa mapambano ya ngumi uliopo Las Vegas, ambao Bondia Thomas Mashari (Kulia) anautamani ujengwe nchini na Serikali ya awamu ya tano.

Bondia Thomas Mashari ameiomba Serikali ya awamu ya Tano kujenga shule ya mafunzo ya ngumi kwa vijana wadogo na ukumbi wa kisasa wa masumbwi ili kukuza mchezo wa ngumi nchini.

Mashari ambaye alishinda ubingwa wa dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kumchapa Muiran, amesema ni aibu kwa mapambano ya kimataifa kuchezwa kwenye uwanja wa ndani wa Taifa ambao hauna hadhi, hivyo wajenge MGM Grand kama ulingo wa ngumi wa Las Vegas, Marekani.

Hadi sasa Serikali imekabidhi ulingo wa ngumi wa kisasa kwa mabondia kuutumia kwenye mapambano yao, lakini bado haijatoa tamko la kujenga ukumbi wa ngumi wa kisasa wenye hadhi za kimataifa, kama ilivyojenga uwanja wa Taifa.