
Cannavaro amesema, katika mchezo wa marudio atakuwa na kazi ngumu ya kupambana ili kuweza kuingia katika hatua ya makundi japo katika mchezo wa awali waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Cannavaro amesema, mpira ni mchezo wa makosa kwani bila makosa hakuna soka lakini ni changamoto kwa timu na watazifanyia marekebisho ili kuweza kubadilika zaidi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumatano ya Mei 18 nchini Angola.
Cannavaro amesema, ametoka majeruhi na amefanikiwa kurudi katika nafasi yake lakini inategemea na kocha anakavyopanga kikosi.