Tuesday , 22nd Apr , 2014

Umoja wa vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko jijini Dar es salaam, wameelezea kufedheheshwa na mwenendo mzima wa Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa UKAWA, James Mbatia kutoka NCCR Mageuzi na Freeman Mbowe wa chama cha demokrasia na maendeleo - Chadema

Wakiongea na Watanzania kupitia vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo wanafunzi hao walioongozwa na kiongozi wao Dorcas Mwasunda wamesema kuwa wao kama wasomi wameona ni vyema kukosoa kile kinachoendelea nchini kwa kutumia kile walichokiita Uhuru wa kitaaluma.

Wanazuoni hao pia wamelaani vitendo vingine vinavyoendelea katika bunge maalum la katiba ikiwa ni pamoja na kudhalilishwa kwa waasisi wa Taifa Wanazuoni pamoja na wanataaluma nchini, huku wakishindwa kutambua kundi la wanasiasa lililounda umoja unaoitwa UKAWA bungeni.