Thursday , 5th May , 2016

Serikali imesema haiweze kuweka programu maalum kukabiliana ya ugonjwa wa Mayoma ambao kitaalamu unajulikana kama Uterine Fibroid unaoathiri kina mama katika uzazi kwa kuwa haifiki hata asilimia 20 ya Wanawake wenye matatizo hayo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangala.

Akitoa ufafanuzi huo jana katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangala, amesema kuna vipaumbele vingine vya magonjwa yanayowasibu wakina mama.

Dkt. Kigwangala amesema ili ugonjwa uitwe ni hatari inaangaliwa ni kundi kubwa kiasi gani linapata ugonjwa si mtu mmoja ingawa alikiri tatizo la wakina mama kupata shida ya kujifungua ina husiana na ugonjwa huo.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa serikali inatenga fedha kwa ajili ya kutoa huduma za afya nchini kwa magonjwa yote ni si ugonjwa wa Myoma pekee ambao huathiri wanawake wanaochelewa kupata ujauzito hadi kufikia umri wa miaka 35.

Majibu ya Waziri huyo hayakuwaridhisha wabunge wengi Wanawake hali ambayo ilimlazimu Waziri wa Wizara huyo, Mhe. Ummy Mwalimu, kusema kuwa majibu hayo ni ya kitaalamu huku akiahidi kuandaa semina kwa wabunge kuelezea suala hilo na kutoka takwimu halisi.

Sauti ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangala,