Naibu waziri wa TAMISEMI,Seleman Jaffo,
Akijibu swali la Mbunge wa viti Maalum Aida Jospeh Kenani, Naibu waziri wa TAMISEMI,Seleman Jaffo, amesema kuwa imebainika kuna madeni feki ambayo yamechomekwa kwa walimu hao kama ilivyo wafanyakazi hewa hivyo serikali inafanya jitihada ya kujiridhisha ili kuwalipa walimu.
Mhe. Jaffo amesema licha ya jitihada hizo wanazofanya lakini serikali inakiri kwamba madeni hayo yataendelea kudaiwa kwani kila siku walimu wanahamishwa na wengine wanapandishwa vyeo kwa hiyo itakua ni vigumu kuyamaliza yote.
Aidha Naibu Waziri huyo ametolea ufafanuzi suala la madeni wanayodai walimu kwa mitihani ya kidato cha pili na cha nne mwaka jana na kukiri kuwa hawajalipa lakini wamefanya kwa lengo la kufanya uhakiki wa matumizi ya fedha hizo kwa kuwa imebainika nyingine huwa zinaishia katika mifuko ya wachache.
Mhe. Jaffo amesema kuwa wameilekeza Mikoa yote ipeleke takwimu za matumizi ya pesa hizo ambapo mpaka sasa ni Mikoa tisa tu ambayo imetekeleza suala hilo ikiwa ni Mkoa wa Mbeya,Tanga, Mara, Arusha,Iringa, Kigoma, Kilimanjaro,Lindi na Mtwara.