Katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad.
Akiongea akiwa mapumzikoni Hotelini, Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad,amesisitiza kutoshiriki uchaguzi huo na kuwataka wananchama wa Chama chake wasijitokeze siku ya kupigaji wa kura.
Maalim Seif amesema kuwa msimamo wa upo pale pale na walishapeka barua kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), pamoja na wagombea wote wa chama hicho ingawa tume hiyo bado imeyaweka majina yao katika karatasi za kura.
Aidha Maalim Seif amesema pamoja na tume kushinikiza uwepo wa ushikiriki wao lakini kamwe hawatoyatambua matokeo ambayo yatapitakana katika uchaguzi huo ambao unarejewa baada ya uchaguzi wa awali wa October 25 kufutwa na mwenyekiti wa tume hiyo kwa madai ya kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu Mkubwa.
Pia Katibu Mkuu huyo amelilalamikia Jeshi la Polisi Visiwani humo pamoja na Serikali kwa kuwakamata wanachama wa chama hicho bila sababu za msingi akiwemo katibu uenezi wa chama hicho visiwani humo na kusema CCM, hawapaswi kutumia nguvu kwa sababu uchaguzi huo utakua hauna upinzani wowote.