Monday , 14th Mar , 2016

Waziri wa Ujenzi,uchukuzi,na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema serikali imetoa kiasi cha shilingi billion 11.2 ili kukamilisha haraka ujenzi wa daraja la mto Kilombero lenye urefu wa mita 384 ambalo linatarajiwa kukamilika Nov 11 mwaka huu.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katikati akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini

Akizungumza na wananchi wa Kilombero na Ulanga wakati akitembelea kivuko kilicho pata ajali mapema mwaka huu na kugharimu maisha ya watu na upotevu wa mali Mbarawa amesema Serikali itahakikisha daraja linakamilika mapema na kuwaondolea adha wananchi wa wilaya hizo iliwaweze kuvuka kwa usalama zaidi.

Aidha profesa Mbarawa amesema kivuko hicho kimetumia zaidi ya shilingi milioni 342 ilikukirejesha tena kuendelea kutoa huduma za uvushaji wa abiria na magari ambapo aliwaomba wananchi wanaotumia kivuko hicho kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria zilizopo ikiwa nipamoja na kulipa nauli.

Kwa upande wao wananchi wa kilombero na ulanga wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa daraja hilo unakamilika haraka kwani kivuko kilichopo bado sisalama na kumekuwa kukitokea matukio mengi ya kuzama kwa kivuko na kupoteza ndugu zao bila sababu yoyote insert wananchi

Nao wafanyakazi na vibarua wa ujenzi wa daraja hilo walijitokeza mbele ya waziri huyo wakiwa na mabango ya jumbe tofauti tofauti wakidai kunyanyaswa na kampuni ya kichina inayo jenga daraja hilo kwa kuwafanyisha kazi bila kuwalipa na mambo yakawa hivi.