Friday , 11th Apr , 2014

Bondia Sukkasem Kietyongyuth kutoka nchini Irani na Bondia Francis Miyeyusho Chichi Mawe wamepima uzito pamoja na afaya zao hii leo tayari kwa pambano lisilo la ubingwa litakalopigwa hapo kesho katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam.

Pambano hilo litakalotanguliwa na Pambano kati ya Bondia Gavad Zohrehvanda kutoka nchini Thailanda atakayepambana na Francis Cheka ambapo Rais wa Shirikisho la Masumbwi ya kulipwa nchin Emmanuel Mlindwa amesema wamefanya jitihada kubwa ili kuhakikisha mabondia wa Tanzania wanapata mapambano ya kimataifa ili kupata uzoefu.

Kwa upande wake Mratibu wa Pambano hilo, Musa Kova amesema kupima uzito kwa mabondia hao ni ishara tosha ya kukamilika kwa maandalizi katika kila Idara ambapo Mabondia haowamejinasibu kuonyeshana uwezo wa kutupa masumbwi wawapo ulingoni licha wa kuonana kwa mara ya kwanza katika ulingo wa Tanzania.