
Mchezaji wa Pool Table
Chama cha mchezo wa pool table Tanzania TAPA kimesema kuwepo kwa ratiba ya michuano mingi katika kalenda ya chama hicho itasaidia kuwapa uzoefu wachezaji hasa chipukizi ambao wanakua hawajapata michezo mingi migumu.
Katibu mkuu wa TAPA Amos Kafwinga amesema moja ya mikakati yao katika kuinua mchezo huo ni kuandaa mashindano mengi ambayo yata ambatana na mafunzo ya sheria na mchezo wenyewe.
Kafwinga amesema awali walianza kwa kusuasua hasa mwaka 2008 waliposhiriki michuano ya Afrika nchini Swaziland lakini mwaka jana mchezaji mmoja aliweza kuweka rekodi kwa mara ya kwanza baada ya kumfunga mchezaji kutoka Afrika Kusini na hivyo kuvunja utawala wa Afrika Kusini katika mchezo huo barani Afrika.
