Chiba
Chiba ametolea mfano wa yeye binafsi kujituma na kufanya kazi ambayo asilimia kubwa ya mashabiki wanaifurahia sasa, ambayo imetokana na jitihada zake binafsi akiwa sasa na nafasi ya kupanda katika majukwaa makubwa kuonyesha kipaji chake.
Chiba kupitia kazi yake ya unenguaji muda mrefu bila kuchoka jukwaani, amekuwa ni moja kati ya wasanii ambao majina yao yanaendelea kushika chati kwa kiasi kikubwa, akitarajiwa kufanya makubwa mwaka huu kwa upande wa unenguaji.