
Kaligraph
Kaligraph amesema kuwa ugomvi wake yeye na Octopizzo si ndani ya muziki tu ila unahusiana na mambo ya binafsi pia kwa kiasi chake, na hivyo kufanya ishu hii kuwa tofauti na bifu nyingine ambazo hupangwa kati ya mahasimu wawili kama njia ya kuvutia watu kusikiliza kazi zao.
Rapa huyu amesema kuwa, licha ya kuwa na bifu na Octopizzo ambaye yupo katika nafasi nzuri kimuziki huko Kenya, anakiri kuwa msanii huyu ana mchango wake katika kufikisha muziki huu mahali ulipo sasa.
