Wednesday , 20th Jan , 2016

Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma zimesababisha maafa makubwa Wilayani Mpwapwa ambapo zimeharibu jumla ya kaya 71 zenye wakazi 332 wa kijiji cha Gulwe na Chiseyu.

Hii ni moja kati ya nyumba za polisi ambazo zimeharibiwa na mafuriko.

Uharibifu huo umetokea baada ya maji kujaa kwenye nyumba za watu na kusababisha baadhi ya nyumba hizo kuanguka na nyingine kujaa maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Mvua hizo zilisababisha mafuriko hayo usiku wa kuamkia leo katika vijiji hivyo na kupelekea idadi ya wakazi hao kukosa makazi ya kuishi pamoja na uharibifu mkubwa wa mali zao pamoja na vyakula.

Akizungumzia maafa hayo jana Diwani wa kata ya Mlunduzi, Orgeness Mchete alisema kuwa mvua hiyo imeharibu jumla ya hekari 47 za mazao ikiwa ni pamoja na kuharibu miundombinu ya barabara.