Tuesday , 19th Jan , 2016

Taasisi na makampuni mbalimbali nchini yatakiwa kufanya kazi zao kwa kulinda haki za binadamu, kutunza mazingira, na kuwajali wafanyakazi wao.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imezitaka taasisi na makampuni mbalimbali nchini Tanzania kufanya kazi zao kwa kulinda haki za binadamu, kutunza mazingira, kupinga rushwa na kuwajali wafanyakazi wao.

Akiongea leo jijini Dar es salaam wakati akizindua Mtandao wa Umoja wa Mataifa unaojulikana kama UN Global Network amesema, Mh. Samiah amesema suala la utekelezaji wa haki za binadamu linahitaji ushiriki wa pande zote, ili sekta binafsi iweze kufanikiwa na kuleta maendeleo endelevu na lazima ijali haki za binadamu ikiwemo kupinga unyanyasaji.

Kwa upande mwingine, Mhe.Samia amesema sekta binafsi zinawajibu wa kufuata sheria za kazi kwa kuzingatia misingi ya Umoja wa Mataifa.

Naye mwenyekiti wa mtandao wa umoja wa mataifa wa Global Network Tanzania Patrick Ngowi amesema watahakikisha watoa fursa ya kusimamia na kutekeleza haki za binadamu pamoja na kusimamia wajibu wa kulinda haki.