Monday , 18th Jan , 2016

Mchezaji anayeorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwa ubora katika mchezo wa Tenis duniani Novack Djokovic amepuuza madai ya udanganyifu katika ngazi za juu za mchezo huo.

nyota namba moja kwa ubora duniani Novan Djokovic katika picha

Djokovic ambaye ni bingwa mara 10 wa gland slam amesema kuwa udanganyifu wa mechi hauwezekani katika tenisi ya ngazi ya juu huku madai ya ufisadi yanaonekana kuzonga wakati wa kuanza kwa michuano ya Australia Open.

Mchezaji huyo ambaye amekiri kukataa pauni laki moja na kumi elfu ili kushindwa katika mechi alipoanza mchezo huo, amesema hatahivyo hakuna ushahidi wa udanganyifu miongoni mwa wachezaji wa ngazi za juu.

Taarifa zinasema kuwa BBC na BuzzFeed imepokea nakala za siri ambazo zina ushahidi wa udanganyifu katika mchezo huo.

Nakala hizo zinaonyesha katika muongo mmoja uliopita,wachezaji 16 ambao wameorodheshwa katika 50 bora duniani wamepelekwa katika kituo cha maadili cha mchezo huo kwa shauku kwamba huenda walikubali kushindwa baadhi ya mechi.