Monday , 11th Jan , 2016

Watanzania wameaswa kuzingatia lishe bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.

wenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane amesema kuwa kumekua na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa hao kitaifa ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa Asilimia 9.6.

Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

Mratibu wa zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David Shungu amesema kuwa wananchi wanapaswa kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na magonjwa yanayoambukiza.