
Waziri Mwalimu ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa adhma ya serikali kusomesha watoto bure lazima iheshimiwe na wote.
Hata hivyo waziri amewakumbusha viongozi wa mikoa na halmashauri kote nchini kutimiza wajibu wao kwa kusimamia vizuri jamii katika suala la upatikanaji wa elimu hasa kwa wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka huu.
Mwishoni mwa mwezi wa pili 2016 maafisa wa maendeleo ya jamii wa mikoa halmashauri na kata wametakiwa kutoa ripoti juu ya wanafunzi ambao wamejiunga na shule mwaka huu.
Pia Serikali imetoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanakwenda shule na kufuatilia maendeleo yao na wahudhurie kwa ufanisi na serikali haitopenda kuona utoro mashuleni kutokana na sababu zinazoepukika.
Hata hivyo serikali tayari imetuma mashuleni nchi nzima kiasi cha shilingi bilioni 18.77 kwa ajili ya kuanzia kutoa elimu bure katika shule za sekondari na msingi za serikali.