Friday , 1st Jan , 2016

Mchezaji wa Kriketi aliyewahi kutumika kifungo jela Mohammed Amir ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Pakistan kwenye mechi ya Twenty20 dhidi ya Newzealand baadae mwezi huu.

Mchezaji wa Kriketi aliyewahi kutumikia kifungo cha jela Mohammed Amir ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Pakistan kwenye mechi ya Twenty20 dhidi ya Newzealand baadae mwezi huu.

Amir alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa tatu waliofanya udanganyifu wa kupanaga matokeo kwenye mechi dhidi ya Uingereza mwaka 2010,kisha mwaka 2011 alitumikia nusu ya miezi 6 jela kabla ya kuachiliwa.

Amir mwenye umri wa miaka 23 pia alipigwa marufuku ya kutoshiriki Kriketi ndani na nje kwa miaka mitano,kabla ya kumalizika adhabu hiyo mwishoni mwa mwaka wa jana.

Chama cha kriketi nchini Pakistani kimesema kinataraji kupata pasi ya kusafiria ya Amir kutoka nchi ya Newzealand.