
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na afisa wa taasisi ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya afya ya macho pamoja na uzinduzi wa utoaji wa huduma za bure za kupima macho unaotarajiwa kufanywa na taasisi hiyo kuanzia leo jijini Dar es salaam.
Kutokana na hilo, Mashayo, amewashauri Watanzania kuwa na utamaduni wa kupima afya za macho yao hasa wale wenye umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea, na amewataka wanaotoa huduma za miwani kuziuza kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wenye uhitaji wa vifaa hivyo lakini hawana uwezo, kuvipata kwa urahisi.