Tuesday , 29th Dec , 2015

Muongozaji wa video hapa nchini Adam Juma amesema wasanii wengi hapa nchini wanaoenda kufanya video za muziki nje ya nchi, wanaenda kufuata conection na mawazo mapya na si jambo baya

Adam Juma ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Rado, na kusema kuwa si jambo baya kwa msanii kufanya hivyo kama ina faida kwenye soko lake.

“I think ubora hatuko tofauti sana lakini pia labda ni mawazo mapya, siwezi kusema sio kwamba ubora uko tofauti, ndio wana vifaa vizuri lakini hata sisi tunavyo, mwisho wa siku it doesn't realy matter wache waende nje wakashoot, kama director najiamini na nina mawazo, na kama itawasaidia kwenye biashara yake kuongeza pesa hiko ni kitu kizuri”, alisema Adam Juma.

Pamoja na hayo Adam Juma amesema anashindwa kuelewa kwa nini video zilizotengenezwa na producer wa hapa nyumbani kutochezwa na vituo vya televisheni vya kimataifa, wakati ubora wa video ni ule ule na zinazo tengenezwa nje.

“Siwezi kusema ni upendeleo na inawezekana ni upendeleo, kwa sababu kuna kazi unaweza ukatuma mtu anakwambia sija download internet bei ghali, lakini sio kama ubora uko tofauti hapana, lakini hata sisi kuna madirector wanafanya vizuri”, alisema Adam Juma.