Tuesday , 22nd Dec , 2015

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini inatarajia kukutana hapo kesho kupitia usajili ambao haujakamilika kwa pande mbili kuweza kukabiliana pamoja na kesi za nyuma za madai kati ya wachezaji na vilabu.

Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema, katika kesi za madai kuna kesi takribani 40 za nyuma ambapo hapo kesho kamati hiyo itapitia usajili wa sasa pamoja na madai mengine kati ya wachezaji na vilabu yaliyotokea katika kipindi cha nyuma ambapo baada ya hapo kamati itatoa taarifa ya walichoafikiana na kutoa maelekezo juu ya yale waliyokutana nayo.

Kizuguto amesema, wachezaji ambao hawakuwa na matatizo yoyote ambayo ni kuwekewa pingamizi waliruhusiwa kuanza kutumika katika mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki iliyomalizika ambapo wale ambao hawakupata nafasi, ufunguzi wao utapatikana hapo kesho.