Monday , 21st Dec , 2015

Serikali imesema itazima simu za watanzania kwa zaidi ya asilimia 40 kutokana na kutokukidhi kwa viwango vya ubora wa simu hizo baada ya mfumo mpya wa rajisi wa namba tambulishi wa vifaa vya kiganjani kuanza kutumika.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy

Akiongea na East africa radio leo Meneja mawasiliano kutoka Mamlaka ya mawasiliano nchini Bw. Innocent Mungi amesema kuwa baada ya kutambulishwa kwa mfumo huo serikali inatoa miezi sita kwa watumiaji wa simu feki na zisizokidhi viwango, kununua simu nyingine kwa kuwa baada ya hapo watazifunga

Bw. Mungi amesema zaidi ya Asilimia 60 ya Watanzania wameanza kutumia mfumo huo mpya na kugundua ubora wa simu wanazonunua na kuwataka watanzania watumie vizuri mfumo huo ili kuepuka hasara pamoja na kulinda simu zao na wizi wa simu za mkononi.

Aidha Bw. Mungi amesema kuwa endapo mtu atatoa taarifa ya kuibiwa kwa simu yake kituo cha polisi na kwa mtoa huduma basi simu hizo zitafungwa kufanya kazi huku akibainisha kuwa na huo ndio utakua mwisho wa wizi wa simu za mkononi kwa Tanzania.