Friday , 18th Dec , 2015

Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) limewasimamisha kazi wafanyakazi wake 10 wakiwemo wahasibu na mafundi kwa kusababisha upotevu wa mapato katika mfumo wa mita kwenye minara ya simu.

Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Felchesmi Mramba

Shirika la Umeme nchini Tanzania (TANESCO) limewasimamisha kazi wafanyakazi wake 10 wakiwemo wahasibu na mafundi kwa kusababisha upotevu wa mapato katika mfumo wa mita kwenye minara ya simu.

Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Felchesmi Mramba amesema jumla ya umeme wenye thamani ya shilingi bilioni 100 milioni 284 na laki 386 na senti 42 uliokuwa umetumika bila ya kulipiwa.

Aidha Mramba amesema jumla ya wateja 30 wamejisalimisha tangu kutangazwa kuanza kwa zoezi la ukaguzi wa mita, ambapo waliokutwa na dosari mbalimbali ni 138, na waliolipishwa faini ni 138 na waliofikishwa kwenye vyombo vya dola ni 37.