Wednesday , 16th Dec , 2015

Staa wa muziki Linex, baada ya kufanikiwa kulishika soko la Afrika Mashariki, hatua inayofuata katika muziki wake katika kuanza mwaka 2016, ni kuendesha gemu mbili tofauti kwa mara moja, akiwagawa mashabiki wake katika makundi mawili makubwa.

Staa wa muziki nchini Linex

Linex amesema kuwa, ameona wasanii wengi Afrika wakifanya gemu mbili tofauti, kwa maana ya kuwatengenezea muziki mashabiki wa nyumbani, na vilevile kufanya muziki akiwa anawazingatia mashabiki wake kwa upande wa bara la Afrika kwa ujumla.