![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2015/12/15/jkt ruvu vs prisons.jpg?itok=kPTbcKGb×tamp=1473305117)
Kibaden amesema, vijana wake wameanza kujituma na wanacheza kwa uelewano tofauti na alivyokabidhiwa kikosi hicho ambacho alikikuta kipo vibaya.
Kibaden amesema, kwa hali ilivyo katika kikosi chake hadhani kama JKT inaweza kushika daraja kama awali watu walivyokuwa wanaiombea mabaya kutokana na kufanya vibaya.
JKT Ruvu imepata ushindi wa pili baada ya Kibaden kupewa jukumu la kuifundisha timu hiyo kufuatia Fred Felix Minziro kuachia ngazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye Ligi.