Aliekua Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Bw, Philemon Mollel
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mollel maesema hakuridhika na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa kwa sababu kulikua na kasoro kadhaa zilizojitokeza.
Mollel amedai kuwa kulikua na gari la diwani mmoja wa CHADEMA, ambayo ilipita baadhi ya vituo vya kupigia kura ikidai kuwapelekea chakula mawakala lakini gari hiyo ilikua imejaa kura feki zilizofanikiwa kuingia katika masanduku ya kura.
Katika matokeo hayo, Godbless Lema wa Chadema amepata kura sitini na nane elfu mia nane arobaini na nane, huku Philemon Molle wa CCM akipata kura elfu thelathini na tano mia tisa na saba,Navoi Mollel wa ACT WAZALENDO kura mia tatu arobaini na mbili,Zuberi Mwinyi wa CUF kura 106 na Mkama Jaralya wa NRA kura 43.
Kwa upande wake Mh. Lema aliwashukuru wananchi wa Arusha Mjini kwa kumrejesha tena bungeni kupitia sanduku la kura huku akieleza kusikitishwa na idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza.