Friday , 11th Dec , 2015

Nyota wa muziki Rufftone kutoka nchini Kenya, ameonekana kuanza kufurahia maisha mapya kama balozi wa mahusiano mema akiunganisha Kenya na Korea, akiwa sasa katika ratiba ya kukutana na viongozi wa juu huko nchini Korea.

Nyota wa muziki Rufftone kutoka nchini Kenya

Rufftone ameonekana akiwa tayari kazini kushughulikia masuala ya msingi yanayohusu uongozi na vijana huku akifurahia ufahari, hadhi na heshima kubwa zilizokuja sambamba na jukumu hilo kama viongozi wengine wa juu serikalini, ikiwepo kusafiri kwa ndege ama jeti binafsi, kutembezwa na limo akipewa ulinzi wa hali ya juu kabisa.

Nyota huyo bado anaendelea na ziara yake kwa sasa, huku kukiwa na matarajio makubwa ya mabadiliko kwa upande wa vijana na masuala muhimu wanayokabiliana nayo kuelekea maendeleo yao, kutokana na matunda ya kile ambacho staa huyu anakishughulikia akishirikiana na serikali ya Korea.