
Katibu Mkuu wa TBA Alferio Nchimbi amesema, timu kutoka mikoa saba zimeshiriki katika mchezo huo ambazo ni Iyunga kutoka Mbeya, Sanya Juuu Kilimanjaro, Mwanza Baseballl Club, Mwanakwerekwe Zanzibar, na wenyeji Dar es salaam kutoka shule za Azania na Kibasila, huku nyingine zikiwa za Tiger na Jians kutoka wilaya ya Ilala na Temeke.
Nchimbi amesema, wameamua kupeleka mashindano hayo mashuleni kutokana na katiba yao kuelekeza kwa wanachama wao namba moja ambao ni vilabu vitakavyoundwa katika shule kwani kunaviopaji vingi vinavyoibuliwa na kulelewa.
Nchimbi amesema, wameanza na shule za Sekondari lakini kwa kuzingatia sheria za kukuza michezo ambazo zinaendana na Nidhamu, Elimu na Heshima hapo baadae wataendeleza mchezo huo kwa upande wa Shule za msingi hapa nchini.