Thursday , 10th Dec , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Mgufuli ametangaza baraza lake dogo jipya la mawaziri lenye wizara 18, huku akiwabakiza mawaziri wa zamani 7

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Mgufuli ametangaza baraza lake dogo jipya la mawaziri lenye wizara 18, huku akiwabakiza mawaziri wa zamani 7 na kuingiza sura mpya katika baraza hilo litakalokuwa na jumla ya mawaziri na manaibu waziri 34 tu.

Aidha, katika baraza hilo Rais Dk. Magufuli ameacha wazi nafasi za uwaziri katika wizara nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Ujenzi pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambazo amesema bado hajapata watu wa kuwakabidhi majukumu ya uwaziri.

Dk. Magufuli amesema serikali yake imepunguza bazara la mawaziri ili mawaziri walioteuliwa wakafanye kazi, na kusisitiza hakutakuwa na semina elekezi ambapo ameagiza fedha zaidi ya shilingi bilioni 2 zilizotengwa kwa semina hiyo kuchukuliwa na kutumika katika shughuli nyingine.

Aidha, Dk. Magufuli akatuma salamu kwa mawaziri aliowateuwa katika baraza lake ambao wanapenda kufanya sherehe wajue wamepewa kazi ngumu na iwapo watafanya sherehe hizo wajiandae na kufanya sherehe pia wakati watakapotimuliwa kazi.
BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri - George Simbachawene na Angella Kairuki

Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri - January Makamba

Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri - Jenista Muhagama

MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri - Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini

Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.

Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria,

Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Dk. Augustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Waziri - Ummy Mwalim

Naibu Waziri – Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

Waziri - Nape Nnauye

Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Waziri – Prof. Makame Mbarawa

Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela