Wednesday , 9th Dec , 2015

Kikosi cha timu ya taifa ya mchezo wa Rollball kinatarajiwa kuondoka Desemba 14 mwaka huu kwenda nchini India kushiriki michuano ya dunia inayotarajiwa kufanyika Desemba 17 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Rollball Noel Kihunsi amesema, wachezaji wanaendelea na mazoezi na hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kutafuta viza kwa ajili ya wachezaji pamoja na viongozi watakaoambatana na kikosi hicho.

Kihunsi amesema, licha ya kukabiliwa na ukata katika chama lakini wamejitahidi kukamilisha mambo yote ya muhimu kwa ajili ya safari ili kupata muda mrefu wa kuweza kujiandaa kwa ajili ya michuano hiyo na kuweza kuipeperusha vizuri bendera ya taifa.