Thursday , 3rd Dec , 2015

Kufuatia kifo cha staa kinda wa kudansi kutoka nchini Uganda, Alex Ssempijja staa wa muziki Eddy Kenzo bado anaendelea kusimamia matibabu ya Patricia ambaye alinusurika katika ajali hiyo.

Msanii wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo akiwa na dansa kinda marehemu Alex Ssempijja

Aidha Kenzo amezungumza na kulaumu taarifa za kuzusha ambazo zilisambazwa hapo awali kuwa Patricia naye alipoteza maisha katika tukio la ajali.

Kenzo ameeleza kuwa, habari kama hiyo hususani kutoka kwa mwanahabari ambaye anafahamika zinaonyesha wazi kuwa si mwanahabari makini kutokana na kusambaza taarifa ambazo hajazichunguza.

Juliana amekuwa ni kati ya mastaa wengi pia ambao wamezungumzia kwa hisia nzito kifo cha Alex Ssempijja, akieleza kuwa kifo hicho kinamkumbusha kwa karibu kifo cha Keron mtoto wake, akiwataja marehemu hao wawili kama mashujaa wake.