
Timu zote mbili zilionekana kucheza kwa kuhitaji ushindi ambapo katika robo ya kwanza IP iliweza kushinda kwa pointi 18-21 ambapo katika robo ya pili Jeshi Stars iliweza kuongoza kwa pointi 21-16 lakini katika robo ya mwisho ya kumalizia mchezo IP waliweza kuibuka na ushindi kufuatia kupata pointi 15-11.
kwa upande wa wanawake Tanzania Prisons ikaibuka kidedea dhidi ya Makongo Sekondari kwa ushindi wa seti za 21-16 na 21-19.
kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wanaume Chui ikaibwaga Prisons kwa 2-1 huku kwa upande wa wanawake Makongo B ikaichapa makongo A kwa seti 2-0.